Premier Bet inaleta Faraja na Furaha kwenye Krismasi katika kituo cha watoto yatima

Premier Bet Tanzania tumeamua kuweka tabasamu kwenye sura za watoto katika kituo cha watoto yatima kilichopo Dar es Salaam. Kampuni iliwapa watoto hao vyakula na vinywaji na vitu vingine vya muhimu kama ishara ya kusambaza upendo kwenye kipindi hiki cha sikukuu.

Kituo hicho kiitwacho Ijango Zaidia, kilichopo Sinza Madukani, Dar es Salaam kinafanya kazi kubwa sana kuwaokoa watoto wanaishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapa mahala salama pakuishi na kujifunza.

Kutilia mkazo jitihada zao, Premier bet imetoa viroba vya mchele na unga na vinywaji mbali mbali, Vifaa vya usafi, kalamu, penseli, vitabu vya kusoma na madaftari. Pia Premierbet ilipata chakula cha mchana pamoja na watoto hao siku moja kabla ya Krismasi na idadi ya  watoto ilikuwa  170 katika kituo hicho. Msemaji wa Kampuni aliongezea.. “Kituo hiki kweli ni cha kipekee, kinaendeshwa na viongozi walio na nia na ari, ambao wanajitolea sana kuwasaidia hawa watoto.

Sisi kama Premier bet tunachukulia majukumu ya kijamii serious sana na tunapenda  jamii tunayoishi nayo. Inampa kila mmoja wetu kwenye kampuni hii amani na faraja moyoni kusaidia watoto hawa na zawadi hizi kwenye kipindi hiki cha Krismasi.”

Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii kuona picha mbali mbali za siku hiyo tukiwa na watoto hao katika kituo cha ljango Zaidia. Bonyeza hapa (Click here) kuifuatilia Premier Bet kwenye Facebook, Bonyeza hapa (Click here) kufuatilia kwenye Instagram na Hapa ( click here ) kwa Twitter.